Pages

Thursday, May 10, 2012

TANESCO yaisamehe Zanzibar deni la bilioni 50/-

Default TANESCO yaisamehe Zanzibar deni la bilioni 50/-

WAKATI Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) likipandisha bei ya umeme kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi kwa asilimia 40, imethibitika kwamba limefutiwa deni lake la muda mrefu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalofikia zaidi ya Sh bilioni 50.

Meneja Mkuu wa Zeco Hassan Ali Mbarouk alithibitisha kufutwa kwa deni hilo alipokutana na waandishi wa habari jana na kusema hali hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbarouk alisema deni hilo lilifutwa baada ya uongozi wa shirika hilo kuwasilisha malalamiko yake ya muda mrefu na baadaye kukutana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na kupitia malalamiko yote na kuonekana kwamba deni hilo halina uhalali wa kuwapo.

Uongozi wa Zeco ulikuwa ukipinga ongezeko la bei ya umeme ambayo iliongezwa mwaka 2008.

“Tunamshukuru sana Waziri aliyekuwepo wakati ule (Ngeleja), alikutanisha pande mbili, Tanesco na Zeco na kusikiliza malalamiko na alikubaliana nasi na kutaka kufutwa kwa deni hilo kabla ya kuingizwa katika kero za Muungano,” alisema Mbarouk.

Alifafanua kuwa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu na sasa Zeco imekuwa ikilipa umeme inaonunua Tanzania Bara kwa awamu, lakini hawana deni linalotokana na malimbikizo au kubambikiziwa.

“Tunalo deni la kawaida tu kutoka kwa Tanesco la kununua umeme…hatuna deni linalotokana na utata wa kubambikiziwa,” alieleza Meneja huyo. Mapema, Shirika la Umeme Zanzibar lilieleza kwamba lipo katika hatua ya kutekeleza miradi miwili ya kuongeza vituo vya kusambaza umeme Unguja na kufadhiliwa na Serikali ya Japan.

Mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Japan ni kwa ajili ya kujenga vituo vitatu vya kusambaza umeme kikiwamo cha Mpendae ambacho kitakuwa kikisambaza umeme katika ukanda wa Uwanja wa Ndege na Chukwani ambayo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kuzidiwa nguvu.

Meneja huyo wa Zeco alisema bado wanaendelea na mikakati ya kutafuta wawekezaji katika miradi ya umeme mbadala kwa lengo la kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.

Source: Habari leo

My Take: Inasamehe madeni wakati yenyewe kila siku inalia njaa na kukopa mabilioni katika mabenki

Utengenezaji wa video mpya ya Chris Brown-Till i die

wiz khalifa,,Big Sean na Chris Brown
 Chris hakujiangala wakti anapiga picha au ndo swaga jinsi alivyovaa mkanda na suruali yake?


Facebook kuweka “Listen button” ya Muziki kwaajili ya Wanamuziki, Wasanii na Makampuni

10th May 2012 Blog 0
Muziki ni moja kati ya vitu muhimu vinavyo tufanya tuweze kutuliza mawazo ya hapa na pale, wakati huo huo kutupatia burudani ya pamoja na marafiki zetu. Iwe ni kwenye concet, klabu, barabarani ukiwa kwenye Daladala, Bajaji au kutoka kwenye simu yako. Lakini hususani tunapenda kusikiliza na kucheza muziki tukiwa pamoja na marafiki. Sasa inakuaje pale ambapo upo kazini, shuleni au nyumabi mwenyewe?
Sasa kwa kutumia account yako ya Facebook unaweza kusikiliza muziki unao upenda wewe pamoja na marafiki zako, na pia unaweza kusikiliza muziki kwa pamoja na Group members wako wa facebook. Kila mtu anaweza akawa DJ kwa marafiki zake na ukajihisi mpo pamoja siku nzima.
JINSI ITAKAVYO FANYA KAZI
Ili kuweza kusikiliza muziki anaosikiliza rafiki yako, Nenda kwenye ile sehemu yaku-Chart (chat sidebar) alafu angalia wale rafiki zako walioko online kwa wakati huo, hivyo kwa wale marafiki zako amabo watakua tayari wanatumia hiyo application ya muziki live kwa facebook yao, itakupa fursa ya wewe ku+Click na kuweza kusikiliza mziki huo, pia hapo hapo kwa hilo group la muziki mnaosikiliza mtaweza ku+Chat wote kwa pamoja na kumwambia DJ wenu aweze kuwapa/ kuwasikilizisha muziki muupendao. Hivyo Rafiki yenu sasa anakua DJ wenu, kwakua anajua mnachokipenda.
Listen button Inavyoonekana wakati unataka kuchagua usikilize muziki wa nanai | PICTURE SOURCE: Facebook Blog
JINSI YA KUJISAJILI KUWA DJ
Sasa unaweza kwenda Turntable.fm | Spotify, Myspace au OMG na kujisajili kama mtumiaji, ili Facebook watakapo izindua hivi karibuni (Mwishoni mwa mwezi huu wa April) uwe tayari umesajiliwa na kuweza kuwaburudisha marafiki zako wote unaowapenda.
JE INA FAIDA GANI KWA WANAMUZIKI WETU TANZANIA?
Wanamuziki wetu wa hapa Nchini Tanzania na East Africa kwa Ujumla, wataweza kuweka “Listen Button” kwenye Fan Page zao, na kuwawezesha wapenzi wao wa muziki kuingia na kuwasikiliza moja kwa moja wakiwa Facebook, na kuwafanya kuweza kuelewa ni nyimbo gani haswa hupendwa na Mashabiki zao.
Mfano wa FanPage hizo kwaajili ya wanamuziki na wasanii kwa ujumla utakua kama unavyoonekana kwenye picha hii hapa chini ambapo “Listen button” itakua hapo chini kulia pembeni mwa Likes.

Mfano wa Jinsi Fanpage ya MwanaFa Inavyoonekana akiwa Msanii wa Kwanza Tanzania Kupata Listen Button Ikiwa Kwenye Majaribio
Ni Muda muafaka sasa kwa wasanii na wanamuziki wetu wa Tanzania kutumia fursa hii kuufanya muziki wako kua Social, ambapo watapata maoni zaidi kutoka kwa mashabiki wao na wakati huo huo kuweza kuboresha kazi zao. Hivyo kuwaongezea wanamuziki na wasanii wote kwa ujumla, kuzidi kupendwa zidi na Fans wao hivyo kuwasaidia kuuza vitu vyao malimbali kama picha, cd, t-shirts, Concert tickets na vitu vingine ambavyo vitawaingizia mapato kutokana na Fans wao.
Sasa unaweza kusikiliza muziki uupendao popote ukiwa online pamoja na marafiki zako
Kwa Msaada Wa PopoteMedia
 mx

Wednesday, May 9, 2012

HIGH VOLTAGE: Mwingereza matatani kwa ugaidi K...

HIGH VOLTAGE: Mwingereza matatani kwa ugaidi K...: Mwingereza matatani kwa ugaidi Kenya  9 Mei, 2012 - Saa 10:29 GMT ...

Mwingereza matatani kwa ugaidi Kenya

 9 Mei, 2012 - Saa 10:29 GMT
Jermain Grant
Raia wa Uingereza ambaye ni mwislamu na mwenye msimamo mkali amefikishwa katika mahakama moja mjini Mombasa, Kenya .
Jermaine Grant mwenye umri wa miaka 29 , alitiwa mbaroni mwezi Disemba mwaka jana kwa tuhuma za kupanga mashambulizi ya bomu pamoja na kumiliki vilipuzi kinyume cha sheria.
Maafisa wa serikali ya Kenya wanasema raia huyo kutoka London, ana uhusiano na kundi la wapiganaji la Al Shabab nchini Somalia, ambaye pia aliwahi kufungwa nchini humo kwa kutokuwa na kibali cha kuingia nchini.
Anashtakiwa pamoja na wenzake watatu ambao ni raia wa Kenya ambapo amekana tuhuma zinazomkabili.
Mwandishi wa BBC aliyepo Mombasa Gabriel Gatehouse ,anasema Grant amefika mahakamani akiwa ametulia.
Waandishi wa habari walifurika katika mahakama hiyo na haikujilikana kama kesi hiyo inaweza kuendelea.
Inaarifiwa kesi yenyewe ingali inakumbwa na utata.
Grant alitiwa mbaroni kwa mara ya kwanza mwaka 2008 katika eneo la mpaka waKenya na Somalia lakini alitoroka wakati alipokuwa mahabusu katika kituo cha polisi.
Duru zinaarifu mtuhumiwa alitoroshwa kutoka kituo cha polisi na kundi la Al Shabab.