Pages

Wednesday, June 27, 2012

Hivi ndivyo alivyokutwa Dr.Ulimboka










Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya mazungumzo.

Dokta huyo aliokotwa akiwa na hali mbaya sana na hawezi kuzungumza.

Tukio hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao hata hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani maeneo mengine yote huduma zimeendelea kama kawaida, isipokuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Madaktari hao wametangaza mgomo usio na kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali kutimiza mahitaji yao, ikiwemo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi pamoja na kuwapandishia mishahara.

Licha ya mgomo huo kuanza kuleta madhara kwa wagonjwa katika siku ya kwanza juzi, kwa madaktari kutofanya kazi katika hospitali mbalimbali nchini, jana hali hiyo ilikuwa tofauti kwani sehemu nyingi huduma ziliendelea kutolewa kama kawaida.
SOURCE THIS DAY MAGAZINE




Wednesday, June 6, 2012

Cheki picha za Millard na Hasheem alafu uangalie pia na picha za Millard na Linah,,Pata picha itakuje Linah akisimama na Hasheem Thabeet

http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/06/Millard-Ayo-Linah.jpg
Millard and Linah
http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/06/310.jpg
Millard an Hasheem
http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/06/116.jpg
Millard and Hasheem
http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/06/Millard-Ayo-na-Linah-1.jpg
Millard and Linah 







VIONGOZIN WA UAMSHO WAZIDI KUJISALIMISHA POLISIN ZAZIBAR

VIONGOZIN WA UAMSHO WAZIDI KUJISALIMISHA POLISIN ZAZIBAR


ZANZIBAR JUMANNE JUNI 4, 2012. VIONGOZI wengine wawili wa Jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, leo wamefika Makao Makuu ya Upelelezi Zanzibar ambako walihojiwa kwa muda kuhusiana na vurugu za wiki iliyopita visiwani hapa kabla ya kuachiliwa.
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amewataja Viongozi waliofika Polisi na kuhojiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamshio Shekhe Mselem Bin Ali, mkazi wa Makadara na Shekhe Azan Ahmed Saidi, wa Mfenesini.
Inspekta Mhina amesema katika mahojiano hayo Polisi walibaini kuwa siku ya vurugu hizo, viongozi hao hawakuwepo mjini Zanzibar ingawa Polisi walitaka kujua zaidi kama wao walihusika katika maandalizi ya awali ya mpango huo kabla ya kuondoka kisiwani hapa.
Wakati wa matukio hayo Sheikhe Mselem alikuwa Pemba na Shekhe Azan alikuwa Uwarabuni kwa matibabu lakini alilazimika kurejea Zanzibar baada ya kusikia hali ya vurugu zilizofanywa na vijana wa kikundi chake.
Viongozi hao wanafanya idadi ya viongozi waandamizi wa Jumuiya hiyo waliojisalimisha na kuhojiwa kwa hiyari na Makachero wa Jeshi la Polisi mjini Zanzibar kufikia sita.
Jana viongozi wengine wanne kutoka katika kundi hilo la Uamsho, walijisalimisha wenyewe Polisi na kuhojiwa kwa masaa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa masharti.
Inspekta Mhina amesema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa viongozi wengine wa Jumuiya hiyo ambao hawajafika Polisi, kufanya hivyo badala ya kusakwa na kutiwa nguvuni kuhusiana na vurugu hizo.
Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, walifika mjini Zanzibar na kuwataka wale wote waliohusika katika vurugu hizo kujitokeza kukabili mkono wa sheria.
Tayari watu 78 wamekamatwa na Polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya vurugu zilizosababisha kuchomwa moto kwa magari na baadhi ya makanisa mjini Zanzibar.
Imeandaliwa na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar

Polisi wapora maiti walioua kwa risasi mgodini Tarime





Polisi wapora maiti walioua kwa risasi mgodini Tarime

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya Mkoani Mara, kupitia askari wake wa FFU limelazimika kutumia nguvu pamoja na kuwatisha kwa silaha wananchi na waombolezaji wa marehemu, Mgosi Magasi Chacha (30), aliyekufa baada ya kupigwa risasi ya moto na polisi wanaolinda mgodi wa North Mara uliopo Wilayani hapa.
Sehemu ya mgodi wa dhahabu wa North Mara, unaomilikiwa na African Barrick Golds
Katika tukio hilo la jana Jumanne saa 5:10 asubuhi, polisi wakiwa kwenye magari manne huku wakiwa wamebeba silaha ikiwamo bunduki aina ya SMG, mabomu ya machozi na marungu, waliwasili kwenye hospitali ya wilaya ya Tarime kuchukuwa mwili wa marehemu Chacha kwa nguvu ili kwenda kuuzika baada ya kuwakamata baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa katika msiba huo.
Mgodi wa North Mara unamilikiwa na kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani ya Barrick Gold, na umekuwa katika mgogoro na wenyeji wa eneo hilo mara kwa mara hali inayosababisha kuwapo kwa matukio yanayohatarisha amani mara kwa mara.
Wakati polisi hao wa FFU waliokuwa wametanda aneo kubwa la hospitali hiyo wakitaka kuchukua mwili wa marehemu, mamia ya wananchi, ndugu wa marehemu akiwemo mkewe (jina lake halikupatikana), pamoja na viongozi wa Chadema wilaya ya Tarime, waliwazuia polisi kuuchukuwa mwili huo, wakitaka lazima taratibu za kisheria zifuatwe na si vinginevyo.
Baada ya viongozi hao wa Chadema, wananchi, ndugu na jamaa wa marehemu Chacha kuchachamaa, mke wa marehemu alikuwa akilia kwa uchungu huku akiwa amekaa karibu na mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti, akikataa polisi kuchukuliwa mwili wa mumewe kwenda kuuzika bila ndugu na yeye kuridhia, lakini askari kanzu mmoja wa kiume alionekana kuanza kumburuza mke huyo wa marehemu kwa lengo la kumtoa eneo hilo ili polisi wachukuwe mwili huo.
Wakati mke huyo wa marehemu akiburuzwa na mmoja wa askari polisi aliyekuwa akitii amri ya mkubwa wake wa kazi (majina hayakupatikana), mwanamke huyo alikataa katakata kuondoka, lakini polisi nao walionekana kumlazimisha hadi baadhi ya nguo zake alizokuwa amejifunga zikidondoka kisha baadhi ya maeneo ya mwili wake juu ya kiuno yakiwa yanaonekana nje, jambo ambalo lilioelezwa na walioshuhudia  kama ni udhalilishaji.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia vurugu hizo, baina ya polisi na ndugu wa marehemu, ambapo polisi walilazimika kuweka chemba risasi za moto katika bunduki zao za SMG, baada ya kuona wametaka kuzidiwa nguvu, ambapo waliwakamata na kuwaweka ndani mwenyekiti wa Chadema wilayani Tarime, Lucas Ngoto.
Viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na polisi katika tukio hilo ni, Katibu wa Chadema wilaya hiyo, Mroni Mwita pamoja na diwani wa Kata ya Sabasaba, Christopher Chometa, huku mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), wilaya ya Tarime, Chacha Heche akiponea chupuchupu kukamatwa kwa madai ya kutaka kuzuia mwili huo wa marehemu usiondolewe hospitalini hapo kwenda kuzikwa.
Marehemu Chacha mkazi wa Kijiji cha Nkende ambaye alikuwa mwendesha pikipiki wilayani Tarime, aliuawa Juni 4 mwaka huu majira ya saa 1:45 asubuhi, kwa kupigwa risasi ubavuni kisha kutokea tumboni na askari polisi wanaolinda mgodi huo wa North Mara, unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, na kwamba jeshi la polisi Kanda maalumu ya Tarime na Rorya imethibitisha askari wake kumuua raia huyo, bila kutaja sababu ya mauaji hayo.
Hata hivyo, baada ya vuta nikuvute hiyo iliyodumu takribani dakika 45, hatimaye polisi walifanikiwa kuuchukuwa mwili huo wa marehemu Chacha na kuuondoa nao hospitalini hapo ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, na kwamba magari yaliyokuwepo eneo hilo yakiwa yamesheheni askari ni PT 2036, PT 1873, PT 1863, T 754 BLF pamoja na pikipiki moja ya doria, huku gari la halmashauri ya wilaya hiyo SM 5241 ndilo lililotumika kuubeba mwili huo wa marehemu.
Taarifa ya jeshi la polisi Kanda hiyo maalumu, iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo ya Kipolisi, Sebastian Zacharia-SSP ilieleza kwamba awali marehemu alijeruhiwa kwa risasi tumboni na askari polisi, kwa madai ya kumkata panga mguu wa kushoto mlinzi mmoja wa mgodi huo, Winchlaus Petro (26).
“Kabla mauti kumkuta alijeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na askari polisi waliokuwa doria eneo hilo la mgodi. Marehemu alianza kumshambulia askari kwa panga na kuikata silaha ya askari huyo mara mbili hata baada ya kuonywa kwa kupiga risasi hewani wakati wa kukamatwa”, ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya polisi yenye kurasa moja.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya wilaya ya Tarime, Nagga Marco ilisema, uchunguzi wake umebaini marehemu Chacha alipigwa risasi ubavuni karibu na mgongo, kisha risasi hiyo ikatokea tumboni.
Kwa upande wao familia na ndugu wa marehemu huyo, akiwemo baba yake mkubwa, Charles Matiko waliieleza FikraPevu kwamba, nguvu iliyotumiwa na polisi kuchukuwa mwili wa kijana wao ni ya kinyama, kwani familia ilikuwa haijaridhia kuchukuliwa kwa marehemu kutokana na ukweli kwamba mipango ya maziko ilikuwa haijakamilika.
Mauaji ya watu eneo hilo la mgodi wa Nyamongo, yanaelezwa kushamiri, ambapo inadaiwa mwaka jana vijana wapatao watano waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, Mei 7 mwaka huu kijana mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Mwikwabe aliauawa eneo hilo la mgodi, na kwamba Juni 4 mwaka huu marehemu Chacha aliuawa pia kwa kupigwa risasi ya moto na askari polisi wanaolinda mgodi huo wa North Mara ambao unamilikiwa na kampuni ya kigeni ya Barrick.
SOURCE;Jamii Forums
Habari imeandaliwa na Sitta Tuma, Tarime

Sunday, June 3, 2012

DIGITAL VIBES-STUDIO YA KISASA ZAIDI NDANI YA MOROGORO

eridelicious ndani ya Digital Vibes

                                                    Gq and Reyd

                                            Baadhi ya vifaa ndani ya studio hio